Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Thursday, March 31, 2011

Vijana Wa Kitanzania Msipojijengea Kawaida ya Kuthamini Dada Zenu, Wote Wataishia Kuolewa na Wazungu.

 Nasikitika kuona kaka zetu wakilalamika dada zao kuolewa na wazungu, wakati wao ndio wanasababisha. 
Kwa ufahamu wangu kuanzia miaka10-11 iliyopita kiwango cha wadada wa kitanzania kuolewa na wazungu kimekuwa kikiongezeka kwa kasi kubwa huku kaka zetu wakibaki kusikitika bila kujua tatizo nini. Utasikia, "wewe na uzuri wote huo, umekosa nini kwenda kuolewa na mzungu."lol! Swali langu, ulikuwa wapi wakati niko single?...Unajua, kwa muda mrefu watu wengi wamekuwa wakihisi kuwa mwanamke yeyote anayeolewa na mzungu ana sifa ya umalaya, bila kuangalia upande mwengine wa shillingi kuwa si lazima iwe hivyo kama wengi wanavyofikiria. Hizi fikira hazina utofauti wa msemo wa kabila fulani wanakawaida ya kuwauwa wanaume zao kwa sababu ya mali, au kabila fulani wanakula mbwa! Samaki mmoja akioza basi sio wote hawafahi. Kadri siku sinavyozidi kwenda tumeweza kuona wadada wanaojiheshimu na wenye elimu bora wasio na sifa ya umalaya nao pia wanaoolewa na wazungu. 
Kuna sababu nyingi sana za wanasichana wengi kuamua kuolewa na mtu mweupe. Kuna wanaona kuwa pale kuna uhakika wa maisha mazuri au kuna matumaini ya kuondokewa na maisha magumu, wengine wanaona wanajua kujali na wanauvumilivu, wengine lengo la kupata watoto chotala, kama sie kwetu usukumani binti mweupe anathamani ya kuchumbiwa kwa ng'ombe 40. Hivyo basi kila mtu na sababu zake. 

Tukirudi kwenye upande wa sababu nyingine kuu ambayo pia kuna uwezekano mkubwa wa wadada wa kitanzania kukimbilia kuolewa na wazungu. Mara nyingi umekuwa ukisikia wavulana (wanaume) wakiwapondea mabinti wakitanzania kwa kuwaita majina mabaya kama vicheche, au hata kuwakosoa kwa kudai kuwa wanatabia mbaya. Ambavyo si lazima iwe kweli, wao usema hivyo kutokana na kujiridhisha nafsi zao, bila kujua dharau hizo zinajenga ukuta mkubwa wa kutenganisha uwezekano wa kukosa mke bora wa kitanzania. Na endapo utokea kuwaowa, bado uwadharau wake zao na kutegemea wao ndio waheshimiwe, bila kujua heshima utokana na heshima. 

Unapomweshimu mtu nae hana budi kukuheshimu pia. Binafsi nina mfano hai kabisaaa,-yupo kaka mmoja ambaye anajulikana (superstar wa bongo). Huyu kaka ni mtu anayejiheshimu lakini anakawaida ya kusema "wasichana wa kibongo wote vicheche". Na alishawi kudiliki kuvunja uwezekano wa kuolewa kwa binti mmoja wa kitanzania. Kwasababu aliyekuwa muoaji ni best yake. Na huwa ana kawaida ya kusema hivyo hata kwa marafiki zake wa kike pia na wasichana anayetoka nao ambao wanajiheshimu, lakini kwake ni vicheche. Na na hakika wako vijana wengi wa namna hii, sasa hali hii sijui kama tutafika kama kaka zetu msipojirekebisha. -Oweni au acheni kulalamika!  
All I wanna say is that, tujifunze kukubali vya kwetu. Vya kwetu ni vitamu na vizuri kuliko, hakuna sababu ya kuviponda kisa...kufurahisha nafsi zetu. 

53 maoni / comments:

Anonymous said...

Wazungu ndio hawana hizo tabia za vijana wa Kitanzania?Wanaume wote ni sawa sema wanaishi tofauti.

Anonymous said...

ukweli utabaki ukweli tu,vijana wa kibongo hawajui kuwaandle wanawake...sasa hivi hakuna mwanamke anayetaka kusikia habari yao hata walioolewa now wanataka kutoka kwenye ndoa na kutafuta wazungu..uvumilivu umewashindaa

Anonymous said...

mmmh we teddy asikudanganye mtu, kumkbuka mke mwema au mme mwema anatoka kwa bwana haijalishi mzungu au mweusi, umesikia halle berry na uzuri wote huo lakini ex wake ni mzungu , bada ya kuachana anasema alitoka naye kama favor , maana yake moyoni alikua anadharau wanawake wa weusi,alitaka kujaribu tuu, ,,, tena usiombe upate lizungu racist, litakua kilasiku linahisi unachofanya unakosea kisa umetokea africa , wako wengi wameolewa na wazungu wanalalamikia sana hicho cha wazungu kuwarekebisha kil KITU,SHUKURU MUNGU KAMA UMEPAATA MWEMA, WAPO WAKAKA WEUSI WAKOROFI NA MAZUNGU AMKOROFI VILEVILE

Rose said...

Hahahaha a ni kweli kaka zetu wana tabia ya kuponda lakini wazungu mmh nao wasumbufu kweli kweli
Wanajua kuganda mtu utasema mama yao. Sasa sijui ni wivu au

Anonymous said...

Hapo dada yangu umesema na ni kweli wanaume wa TZ nao siku hizi imekua too much. Mwanaume anatoka na wewe afu hapo hapo bado anaenda kukutangazia mengine sijui ndo wanajiona ni maplayers sana. I have a live example ya hayo unayosema na kweli kweli wajirekebishe hata mi nikipata nafasi ya kuolewa na mwanaume mwingine ambaye c Mtanzania then ntafanya hvyo. Sawa wacha waseme vicheche, ss wamejuaje kicheche kama wao wenyewe sivyo na kama ukicheche c nafanya na wao wenyewe au!? Men are all the same jamani and such is life!

Vina said...

I am with my mzungu coz we get on well and have love and respect for each other! I would have marry him even if he was Mtanzania, black, green or purple...lol

Anonymous said...

nakubaliana na anonymous wa kwanza!
Wazungu wanatabia chafu chafu chafu kuliko...
Mume bora na mwema hutoka kwa Mungu ni kweli..

Wanaume mama yao mmoja...

Hata kuita wanawake vicheche na wenyewe huo mchezo wanao. Yani nina ushuhuda mwingi sana kuhusu hizi ngozi nyeupe.

Tofauti wengi wao hutulia wakifika miaka flani ni asilimia chache ambao utakuta hawajatulia tofauti na kaka zetu wenyewe moto juu.
mama marcus.

Anonymous said...

nampenda mzungu wangu namie sio kicheche.

Anonymous said...

kweli teddy lakini hio list hapo ni new wazungu wives most of the couples wamepata wazungu juzi tu ingekua vyema tungewauliza wake wa wazungu waliokuwa na wazungu sio chini ya miaka 5 au hata wale wanaoishi kinyumba hapo ndio utapata jibu makucha ya mtu hujitokeza baada ya miaka mitano mtu anakua comfortable ila under 5yrs mahusiano bado machanga wao wanafagilia kila kitu wanafikiri mzungu mpole subiri miaka mitano ipite hasa kwa wenzetu wazungu wanapenda akufahama vizuri kati ya miaka 5 hapo ndio utajua kama mzungu ni mwanaume

Anonymous said...

heee man wako mtamu

Anonymous said...

mbona umetoa favourite coupe yangu mbona sikuelewi!!Jana ilikuwepo mbona leo naona wengine? Ilikuwa chini ya Miriam, vp dada?

Mdau kutoka Uholanzi

Teddy Kalonga aka "TK" said...

Nilikosea kuandika jina la mwisho. Imebidi niitoe haraka ili kurekebisha. It's back on now.

-TK

Anonymous said...

asante sana Teddy!! sasa umenifurahisha sana. Mungu akubariki. Na huyo mdau anaesema wazungu wanaonyesha makucha baada ya miaka 5 hajui. Maana hapo hizo couple nyingine ni za miaka mitano sasa sijui unaongea nini!!!

Mdau wa Uholanzi

Anonymous said...

We Teddy na hao mabinti wenye kushupalia wazungu ndio deal acheni kujidanganya. Hivi mnajua divorce rate ya couples za kizungu ama mnatania?? 75% ya ndoa zao huishia kwenye divorce. Tena basi wanayo mambo mazito mno- kwanza mzungu anaweza kuamka tu siku akakwambia mimi ni gay sina tena feeling na wewe. Wengine hulala na watoto wao (sexual abuse) huabuse watoto wao wa kuwazaa haijalishi wavulana ama wasichana- ukiangalia tv za huku ulaya utaona hizi habari kila siku, nadhani kwavile kwa ulaya ni vigumu kuwa na housegirls kama nyumbani basi wababa kwa kukosa mahousegirl huelekeza nyege zao kwa watoto wao. Yani kama wadau wachache waliosema mume mzuri haijalishi rangi bali ni baraka kutoka kwa Mungu. Believe me in this.

Anonymous said...

Hii mada naona km yakizamani,mwanamu awe mtz,au taifa lingine lolote wote ni sawa juu hata mademu wa kizungu wengine wanaona km wanaume hawafai.
Mapenzi cku zote hayachagui thats wat a knw uwe na mzungu usiwe nae doent matter

Anonymous said...

Jamani, ombeni waume wema na mtapewa. Mzungu, Mweusi, Asian, wote ni binadamu jamani, hizi mentality za wapiiii??? Hivi mbona mnamchanganya kila mtu??? Mnajua it's all about the people you surround yourselves with? Hao mnaowapata wanaowadharau ndio group zenu hizo, hebu spread your wings muone. Msikandamize watu kwa kuwa rafiki zenu wana tabia mbovu. SIO WANUME WOTE WA KITANZANIA WANA MISTREAT WANAWAKE, PLEAAAASEEE!!! I have my Tanzanian King who treats me like a QUEEN. Sio Mzungu wala nini. Kama umepata mume mwema, shukuru Mungu, awe MTanzania, MZungu or whatever, ok???

Anonymous said...

wanawake mnao watetea wanaume wa kibongo acheni ukweli mnaujua....ni watu wasiojua nini thamani ya kupenda uongo na uhuni ndo chakula chao..hapa tunataka wabadilike hivyo ukianza kutetea sio kama utakuwa unasaidia bali utakuwa unaongeza matatizo

Anonymous said...

Yaani hii mijanume ya kibongo haifai na inatia tamaa..kuna jamaa mmoja maharufu na heshma zake lakini mambo hanayo yafanya yanatia kinyaa...yaani kamdanganya mdada wa watu wameoana kmpa mimba na kamtelekeza baada ya mdada kuzaa,,na mtoto kukua karudi tena eti warudiane mwanamke kamsamehe kwa kujua yameisha alivyomgeuka na kumtenda ni zaidi ya mara ya kwanza yaani kabeba kila kitu na wala hajamuaga kaenda kutangaza kwa watu hamtaki na wala hana haja naye wala mtoto na ni mtu anajina kubwa tu bongo,ukimuona hata umdhanii yaani ni utumbo mtupu

Anonymous said...

teddy unakosea kama mwanamke hataki kujishughulisha halafu anapenda vya kupewa na akiona jamaa hana hela anamdiss wanawake ndio wengi wenye tabia hii ya kiwadharau wanaume nadhani hata prof jizze alishaimba zali la mentali,pia ile ya yule aliyemtoa kijijini kisha akamgeuka,kama mwanamke anjighulisha na tunasaidiana wote mi sina tatizo ila kama ana tulia kama bwege,unadhani hata hao wazungu watawabeba?

stellah said...

Anonymous said...

ukweli utabaki ukweli tu,vijana wa kibongo hawajui kuwaandle wanawake...sasa hivi hakuna mwanamke anayetaka kusikia habari yao hata walioolewa now wanataka kutoka kwenye ndoa na kutafuta wazungu..uvumilivu umewashindaa
March 31, 2011 6:42 PM

ni kweli baadhi hawajui ku-hanndle lkn sio wote...na sio wote walioolewa na weusi wanataka kutoka kwenye ndoa zao..mie nina furaha na amani kwenye ndoa yangu na Mume wangu Mswahili Mtanzania mwenzangu!!so inategemea

Anonymous said...

kwa bongo ukiwa na mzungu unafagiliwa lakini kwa huku ulaya unachekwa maana wahesabiwa siku the fact tunahigh divorce rate tatizo sio lamzungu mabinti wengi wakibongi niwazembe wanakimbilia tu kuolewa mtu humjui vizuri date hapo hapo harusi hapo kwa hapo ujauzito hapo kwa hapo?couple ya kizungu wanadate mda mrefu bila commitment why because love takes time understanding,trust culture differences etc sisi watanzania nikuvamia tu ndio tunajikuta divorce kila siku sio kwamba mzungu anabadirika ni sisi hatujajenga mahusiano bali tunakimbiria ndoa show off mara tuzae faster hatuna misingi ya maisha mtu akipata tu mzungu haraka tunajenga our fantasies wedding etc any mzungu comes u way we assume he's mr right?lazima atakuja kukuzarau unamlazimisha mwanaume akuoe nawakati masikini wala hakujui vizuri mwenyewe hana mpango that's the fat fact

Anonymous said...

kuna wanawake wengine wanapenda kuwatetea wame zao hata kama wanapigwa na kutolewa ngeu lakini wanasifia tu,kuna mama angu mdo alikuwa nanyanyaswa sana na mume wake,kupigwa,kudhalilishwa kwa matusi hata mbele ya wafanyakazi na watoto tena muda mwingine mwanamme anamtuma akamtongee mwanamke anayemtaka ili alale nae na anafanya hivyo..yaani alikuwa akishauriwa achane na huyo mwanamme hataki ndo kwanza anamtetea so jiulize kuna wanawake wangapi kama wao? wanamme wa kibongo kwenye 100 labda mmoja tu ndo anayejua mapenzi nini na siye wanawake tufunguke tuache kutetea ujinga!

Anonymous said...

kuna story ya yule dada aliyemfumania mume wake na mwanamke ndani lakini ndo kwanza anamdhalilisha mwanamke mwenzie na kusema tukimaliza tunaenda beach na mume wangu tukayamalize saa nyingine sie wanawake ndo tunawapa kichwa hawa wanaume wetu kufanya mambo ya ajabu...lazima tuwaonyeshe kama hawatujali wapo wanaoweza..sasa ni mapinduzi alisi,ukimwaga mboga namwaga ugali lol

Anonymous said...

lol azungu bana wako poa me mme wangu mzungu na he dude bows for me kila kukicha...wakaka wa kitanzania sina noma nao ila i prefer wazungu bana

Anonymous said...

Wadau wote mliosema ni kweli mwanaume awe mweusi awe mweupe inategemea na tabia yake sio wote wema na sio wote wabaya,i hav been married to an american men for over four yrs now lakini plz ana mapenzi na maudhi pia,tena these guys wana tabia mbaya ambayo huwezi eka hadharani afadhali ya black so tujidanganyike na wadhungu kuwa ni wema the only thing is wanajuwa kucare than african men.,,,,,flora

Anonymous said...

wazungu ni watu wa ajabu sana hawaeleweki mtu unaishi na mzungu mnapendana anaonesha interest ya afrika etc unamuona mpole siku moja akija kukuonesha makucha na anakulistia kila ulicho fanya maneno uliosema miaka mwenzio anakumbuka hapan chezea mzungu wewe ukikimbilia kwashow off fulani kaolewa basi na mimi niolewe sijui ukimblie makaratasi au manufaa binafsi yeye anajua ila hakuoneshi lakini ipo siku ataongea i have been there 10ys na mzungu hunielezi kitu hapo msijishauwe mkifikiri mumepata ukweli mumepatikana mzungu atakutegea pabaya sana ndio akuoche they are smart wapole wanakusoma tu miendo yako sio wajinga hao

Anonymous said...

dunia ya leo ukipata mme bora ni unashukuru mungu, awe mzungu, mwafrika,muhindi etc... na sio kwamba wazungu wote wanatabia nzuri same applies kwa wanaume wakibongo sio wote wenye tabia nzuri. tatizo sisi wasichana tunataka ma sharobaro, wenye gari na pesa mwishoni tunabaki tunalia hao ndo wanao cheat!
mapenzi ya kweli yalikua zamani siku hzi ukipata unnashukuru mungu kwa zawadi aliyokupa.

Anonymous said...

White man? an't got nothing compare to a black man.
Whatever! some people they wish if they were white.Stop acting white.Stop being a gruppy

Anonymous said...

Wanawake wengi wanapenda wazungu kutokana na sababu tofauti inatofautiana.1. love,makaratasi,wengine wanapenda kuzaa ili wapate machotara, umasikini wanaona wazungu ni bora watafaidika, Wengini kufuata mkumbo maana masister du wengi wanatoka na wazungu kwa hiyo wanajiona akiwa na mzungu ataonekana yuko juu. wengine wanatoka na wazee old enough to be their babu ili mradi ni mzungu.

Anonymous said...

Jamani miaka mitano pia bado uko honeymoon msijishaue mkasema miaka mitano ndio unamjua mtu. Unaweza ukakaa miaka hata 10 na bado usimjui mtu vizuri so usiseme wewe umekaa miaka mitano na bwana wako ndo unamjua vizuri nipishe mie,hapo cha muhim kama walivyosema wengine uombe upate mume mwema haijalishi rangi wala kabila.

Anonymous said...

Haya mambo jamani, mimi mzungu simtaki hata kwa kutafutiwa kwanza wachafu. Hapa kwenye hizi picha za couple's kuna mzungu mmoja anamahusiano na msichana ambaye ni jirani yake na wako ulaya hajui tu . Jamani mfungue macho wanzungu pia wanacheat:) Poor girl. Kweli usiibanie hii anatakiwa kujua.

Mohamed:(

Anonymous said...

tatizo watanzania tunapenda mashindano ukiona mwenzio kaolewa na mzungu anaishi vyema na wewe utafanya juhudi upate wako utaspeed up maisha ili umshinde mwenzio kumbe unajiumiza mwenyewe usifikiri bahati ya mwenzio ni yako wenzio wametoka mbali wewe unakuja na speed vitu vizuri hafitaki haraka wasichana wakibongo wengi sana wanadhalilishwa na wazungu wanajitahidi kushow happy face lakini mateso yao wayajua wenyewe moyoni many are unhappy infact 5%only are happy na 95%are un happy wakijikuta hawawezi kurudi bongo amekimbilia kuzaa mastress ugenini na ulezi mmmmmmmh mabinti fungueni macho

Anonymous said...

tehe tehe tehe, nimeshika meno yasingoke hapa, tehe tehe tehe, teddy hizi topic uzilete mara nyingi, tehe tehe tehe

HAGGAI said...

kama wazungu wana tabia nzuri mbona divorce rate kwao ni kubwa ...inakuwaje....halafu dada zetu badilikeni mnataka mno vya kuletewa hamtaki kujishughulisha...hili nasema kwa uzoefu wangu katika ndoa...maisha ni kuijishughulisha sio kutafuta wapi pa kupumzika

Anonymous said...

Hakuna lolote hapo naona blah blah na story za uzushi...wazungu wanjua kutake care bwana asikwambie mtu nyie ongeeni lakini moyoni mnakubali

Anonymous said...

Huyo bi chaumbea anayesema kuna mzungu kacheat kwenye hizo couple aache umbea kama hanajiamini amtaje huyo mtu,inaelekea hata hawajui wazungu vizuri,kwa taarifa yako mzungu akikuchoka anakwambia na kila mtu anaendelea na mpango wake,sio ndoa zetu za kibongo mkioana ndo mpaka kufa hata ukimfumania mumeo na dada ako bado unang'ang'ana tu

Anonymous said...

ME MSEMEE MKICHOKA MJAMBE...MZUNGU AKITOKEA NA KUNITONGOZA NINAYE NILIVYOTENDWA NA HAWA WANAUME WA KIBONGO SITAKI KUSIKIA KABSAAA

Anonymous said...

Hapa kuna kama one couple, they only stay togehter but they are not married. Huyu dada ameshapiga kelele na kuolewa wapi? adi ameishia kujivalisha pete mwenyewe...Wazungu pia ni wakorofi jamani hawawezi kuoa hivi hivi utabaki tu naye ndani ya nyumbaaaaa...TK your lucky sweet.
But no matter what wanaume wote ni sawa siku hizi, si mweupe,njano, mwekundu, black or brown.....

Flora from USA.

Anonymous said...

Divorce rate ni kubwa kutokana wa mapenzi yao ni ya kweli ikitokea mmeshindwana ki ubinadamu si kila mmoja anachukua time zake,sio kama wanaume wa kibongo mkioana hata akunyanyase vipi bado utalisha matako,kuna wengine wanafukuzwa na wame zao hawaondoki na kuna wengine hawawezi kuachana kutokana na kiapo walichokula kanisani,na huyo anayesema wadada wapunguze vya kupewa kwa wazungu ni wazi hawajui hawa watu wake wa wazungu wanapiga mzigo kama hawana hakili nzuri hakuna cha kuletewa wala nini kama wanawadanganya wanapewa vya bure ndo mjue waongo

Anonymous said...

mwanume ni mwanaume hakuna cha mzungu wala mbongo aliosema wazungu hawacheat ni nani?wengi wao ni honest lakini kuna cheaters pia kazi yao kudate online huku anamwanamke nyumbani status single na mapicha kutuma mtu anakutongoza online nawakati ameowa kweli kutwa yuko online alafu mtu asema anahappy marriage?? kwa mzungu haijalishi miaka 5 au 10 akichoka goodbye utabaki na hao chotara ombeni mungu asitiri ndoa zenu sio mseme mzungu ni bora the devil you know is better(mbongo mwenzio)then the devil you don't

Anonymous said...

TK ulichokiandika ni sahihi kabisa, wabongo kazi! Nataka niwasiliane na wewe nitumie e-mail kwenye dfulla@gmail.com

Anonymous said...

Jamani jamani jamani...wanaume wakibongo matesooo tena matesoo,,sitetei wazungu sababu siwajui,bali nasema ukweli,nimeolewa ninayoyapata humu ndani aibu hata kuadithia

Anonymous said...

Tk niliteseka na mbongo nikaja kupata mzungu akanipenda mapenzi ya dhati jamani sikujua mapenzi matamu kama niliopata kwa mzungu nisikohoe kila ninachotaka napata alinisaidia mapaka familia yangu alipendwa na kila mtu jinsi alivyokua charming alipenda sana bongo yani sitakuja nisahau raha niliopitia tukapata na watoto nyumba yakifahari magari jamani kweli dunia ni mapito nchi gani sukufika nimetembea weeee ila siku moja mzungu tk alikuja kubadilika akawa ananitesa alianza kunisimanga kama mbongo na zaidi matusi yanguoni wewe masikini u r nothing without me sijui maneno kibao kosa sina nilikua najituma nakazi yangu na elimu akawa ananilala kwa lazima akanisusa watoto aliniambia hakupanga kuwa na watoto hakutaka majukumu nawakati aliwapenda watoto sana lakini alibadilika kama shetani nashindwa kuelewa tk after miaka 13 kanigeuka akanifukuza na watoto nyumba kumbe alaniandikisha sina share?gari jina lake?kumbe alinichota akili tk mwezenu niliteseka nikarudi square one alinipokonya kila kitu ila amelazimishwa kuwalipa watoto hapo nashukuru but hana mapenzi nao navumilia kwasababu ya watoto nawork 7days a week sina vacation nahisi kufa saingine natamani nijirushe ila namuogopa mungu na watoto wangu nashindwa kurudi bongo sina hata kabanda na serikali hainiruhusi kuhama na watoto kwani ni citizens wa huku sasa nitakuja kufa na mawazo kurudi kwetu nashindwa najuta kuzaa nilifanya haraka niliogopa ataniacha jamani nisaidieni mawazo hivi sisi wa bongo tunaoachika na wazungu na tumazaa serikali ya bongo haina haki na watoto wetu?sio mimi tu wapo wengi wanaoteseka mpaka wanapata depression wengine wanakuwa alcoholic watu wanachanganyikiwa asante

Teddy Kalonga aka "TK" said...

(Tears) your story made me cry:( I'm so sorry to hear that. As some of you have said MUME BORA UTOKA KWA MUNGU, that is what I believe too.

Anonymous said...

TK ni hivi,mzungu akimpata msichana wa Kibongo lazima atampenda sana kutokana na maadili.hawezi kumpata mzungu mwenzake akapata heshima ambayo msichana wa kibongo unampa like kumsikiliza au kumpikia au kumfulia nguo n.k. na hamna siku utamnasa kibao au kummwagia bia/wine/whiskey usoni. lakini mzungu mwenzake au mmarekani mweusi anaweza mnasa kibao mbele ya kadamnasi au kutupa nguo zake nje au kumtukana mbele ya wazazi na ndugu zake, upo hapo?sasa kwa mazingira hayo mzungu yoyote atakupenda kwa sababu tangu aanze ku-date hajawai heshimiwa,Otherwise mzungu hana tofauti na Mtanzania au mtu yoyote.I am glad nimejua hilo baada ya kuja Marekani,nilikuwa na perception tofauti wakati nipo bongo.mengi majinga tu na ma-racist especially wakijua umetoka Africa, ni mazingira ya maendeleo ya nchi zao yanawafanya waonekane kama wa maana zaidi kwa dada zetu lakini hamna kitu. TK nimekusifu umevuta kijana lakini chunguza wengi wamekamatia mazee yanayomalizia starehe kabla ya kufa.sasa zee la miaka 60 plus kwa nini lisikuheshimu? hapo ni simple mind tu wala huitaji kuwa scientist.

Anonymous said...

wewe Anonymous umeshindikana unafikiri utasema watu na wenyewe hawajui?sio kila kitu cha mtu ukijue wewe una ushahidi gani kuwa kajivalisha pete mwenyewe?mfa maji wewe kweli huishi kutapatapa..na bado naona utaumia vibaya mno mwaka huu jua lako linalokuweka duniani usingoje hata watu wakishikana shikana uwambiwe..huoni aibu kusema mtu na mwenyewe anakujua?get a life if you dont have one.

Anonymous said...

Umugabo wawe numubeshi

Anonymous said...

Anony pole mpendwa ila kama ulivyosema tuko wengi tunaoteseka kwenye ndoa za wazungu mimi nilikuja kusoma wabongo wakanishawishi nitafute mtasha nipate makarati kweli nilihangaika on dating sites nikabahatika lakini alikua mkubwa sana kwangu ukituona ni vichekesho lakini nataka maisha sio sura au umri niliteseka sana ilifika kipindi nilishindwa kurenew visa so had no damn choice tuliona kisiri nikashika mimba hata marafiki zangu hawamjui naogopa watu watatucheka mtasha anamasimango huyo na mchoyo kupindukia mtu anahesabu chakula na hapendi nipike vyakula vyakibongo madai garama kutwa amenuna nimevumilia ni maisha kuna siku akaniambia ananunua cottage out of town ndio kwaheri mume akawa anaishi huko kila weekend hana hamu na mtoto wala mimi tena nikimuomba anisaidie mtoto analalamika na kugomba asema yeye hakutaka watoto anapiga makabati na kurusha vyombo asema nimeharibu maisha yake niko selfish naogopa kuna siku atanipika vibaya huwa ananirushia kiti kwa hasira na hataki nitafute babysitter anagalau anisaidie huwa anamuliza mtoto kama nilimuacha kwa rafiki zangu nimembembeleza tuende bongo nimpeleke mtoto nyumbani aniambia kuna malaria na kipindupindu sijui nini maneno kibao hataki niende asema nitakimbia na mtoto anafuatilia bajeti yetu ya chakula matumizi jamani utumwa haujaisha nimechoka roho inauma nilifanya uamuzi wakijinga hata wazazi nyumbani hawakupenda nimeolewa mtu simjui na bila ya wazazi kuhudhuria sijui ndio chanzo ananidharau anaona kama ameniokota sina kwetu hawajui wazazi wangu?nateseka na malezi mimi na mtoto pekee najiona kama vile single mother mwenzangu katukimbia huwa akija mpaka mtoto anakosa raha jinsi alivyokuwa mkorofi na hizo pombe akilewa atanitukana msiombe wazungu ombeni mume mwema

Anonymous said...

Pole sana dada kwa story yako, mimi niliishi pia na mzungu miaka 12 na alikataa tufunge ndoa na wala hakutaka tuongelee hiyo topic. Wazungu ni rangi tu wengi wanawaweka wakina dada ndani kama housegirl wao.
Nilikuja kuolewa na mwafrika mwenzangu na tunaishi kwa mapendo miaka 5 sasa:)

Anonymous said...

Uzuri wa mzungu akupende mwenyewe sio ujitongozeshe au kujiweka..ukipendwa mbona utaona raha unapapalikiwa kama queeen,lakini ukiforce mapenzi mbona utakiona cha moto!

Anonymous said...

Mwanaume mweusi ana thamani.Wazungu hata dini hawana wakina dada muslims mliolewa na wazungu dini ya kiislam mnaifuata? hapana. Wengi wamebaki kujipa majina kwenye facebook, Mrs L married/engaged and Mrs R married. The truth is muache kusifia wazungu wenu wachafu. wakina dada wa Europe acheni mashauzi.
Black men they know how to handle a woman lol.

Anonymous said...

Here is only one couple who are not married and its normal, they love each other so much. She is a newly mom and she is famous and very pretty. Put a ring on her own finger it does'nt bother you people Even she can stay with him 100 yrs. Go Miss Earth Go Mama Iris.
We love you as you are and your skin wow! Natural black beauty:)
Black men are sweet but white men are the sweetest:)

Anonymous said...

''Get a life if you dont have one''. I agree with the ananoym who wrote this. Mama Iris ni mzuri, famous and Inteligent with her baby girl huwezi amini katoka kuzaa aliyorudi inshape. Akijivalisha pete ni ni kuamua kwake, cause anaogopa hao wakaka zetu hawaachi kukutongoza tena wakiona dem bomba. Huyu dada ni mzuri. From Miss to a Model. Akitaka olewa ni anytime na hanazo so hapa hakuna kumtegemea mzungu life is equal. Wanaume wa kibongo wamezoea kuhonga ndio akuoe.
Go Miss Odemba. We love you

Miss East Africa
Scotland.

Total Knockout Search!!

Custom Search