Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Sunday, March 20, 2011

Rais KIKWETE: Viongozi wa Dini Msichoke Kumkemea Mtu yoyote anayetaka Kuwagawa Watanzania kwa rangi, Kabila, Dini, jinsia na Maeneo Watokayo!

 “Napenda kutumia nafasi hii pia kuwaomba viongozi wa dini muendelee kufanya kazi ya kulilea taifa letu kiroho na kimaadili. Natambua ugumu wa kazi hiyo katika dunia ya leo ya utandawazi ambako maadili mema ya jamii pamoja na mila na desturi zetu havionekani kupewa thamani kubwa. Siku hizi mtoto mdogo kumtukana mtu mzima au watu wazima kutoleana lugha chafu, na kutositiri maungo, havionekana kuwa mambo yasiyofaa.”
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewataka viongozi wa dini kuongeza kasi yao katika kulilea taifa kiroho na maadili katika dunia ya jana ambako maadili mema ya jamii pamoja na mila na desturi havionekani kupewa thamani kubwa.
Aidha, Rais Kikwete amewataka viongozi wa kiroho kuendelea kuwahimiza Watanzania pamoja na viongozi wa siasa kuvumiliana kwa tofauti za rangi, kabila, dini na siasa na pia kuendelea kuombea amani na utulivu wa Tanzania na upendo miongoni mwa Watanzania. 

Vile vile, Rais Kikwete amethibitisha, kwa mara nyingine, azma ya Serikali yake kuendelea kushirikiana na taasisi za dini katika kuboresha huduma za kijamii nchini za elimu na afya kwa sababu katika hilo shabaha ya dini na Serikali haitofautiani.
Kwa habari nzima bofya hapa=>HAKINGOWI

Source: Hakingowi

0 maoni / comments:

Total Knockout Search!!

Custom Search