Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Friday, January 22, 2010

Swali Kutoka kwa Mdau wa Total Knoout!!...

SWALI:
Hello Teddy,
Natumaini upo mzima, nilikuwa napenda uzungumzie kuhusu foundation kwenye blog yako. Mie sijawahi kutumia foundation ya aina yoyote, nilikuwa sipendi tu maana natural ni mrembo tosha. Sana sana wanja na lipstick natumia.
Sasa mpenzi nimeolewa hivi karibuni, si unajua tena siku ya harusi nikapakwa foundation basi nikaonekana ni mrembo zaidi. Basi shemeji yako ameniambia niwe naweka hiyo foundation. Si unajua tena inabidi nimrizishe mzee,tatizo langu ni kwamba mie ngozi yangu ipo soft and clean naogopa kupaka hizo foundation kwa kuwa naona kama zitaniletea chunusi.
Najua wewe ni model hivyo utaweza kujua foundation ipi nitumie ili isije niletea madhara kwenye ngozi yangu hii ya uso. Mie nina light skin ambayo ni combination skin.

Swali la kizushi! Hivi wewe unatumia foundation gani? Huwa inakutoa mwaaaaaaaaaaa!! Have gud time & take care!!

Pretty Noel

JIBU:
Hello Pretty,
Ahsante kwa swali lako zuri. Kwanza hongera kwa kupata mwenza na hongera kwa kuwa na ngozi nzuri. Kwa kawaida make-up ni kweli zinauwezo mkubwa wa kuharibu ngozi, na hii ni kutokana na kutoosha sura yako vyema wakati wa kuondoa au hata kutumia make-up isiyo na ubora. Lakini pia make-up uongeza unadhifu wa mtu ki'urembo.Mimi binafsi katika maisha yangu ya kawaida nimekuwa nikitumia L'Oreal foundation,...
Lakini nikiwa kazini huwa napakwa M.A.C. kwasababu ni nzito na inaokana vizuri kwenye professional cameras.
Do:Jaribu LO'real... na kwakuipa nafasi ngozi yako kupumua, paka kidogo. Hasa hasa sehemu ya chini ya macho, kati ya mdomo na pua(sehemu ya mustachi.lol!) Na kidogo kwenye paji la uso. Waweza kutumia brush au sponge ya kupakia...
...lakini hakikisha unasafisha brushes zako kwa kutumia shampoo angalau mara 1-2 kwa wiki. Tumia tishuu za unyevu nyevu au facial cleanser cream kuondoa vyema make-up usoni.
Don't:
Kamwe usithubutu kulala na make-up. Kamwe husithubutu kujishikashika usoni wakati umepaka make-up, kwasababu mikono yetu siku zote hubeba (bacteria)vijidudu visivyoonekana kwa macho.

Karibu kwenye ulimwengu wa make-up Pretty Noel.

3 maoni / comments:

Anonymous said...

make up zinatofautiana kutokana na skin complexion. L`oreal inafavor zaidi wenye lighter skin tone..MAC kwa upande wangu inafavour all black skin tones na mimi na watu wengine wengi walioitumia wanaisifu. Usinunue tu hivihivi nenda dukani wakufanyie testing uchukue inayomatch kabisa na wewe. Usichukue a shade lighter or darker..One secret paka kidogo tu usionekane cakey..malizia na face powder a bit darker in shade(bronzer..) vizuri uipake na brush kubwa..all da best

pretty Noel said...

Ahsante sana kwa maelezo yako,nimekuelewa my dear.
Be blessed.

Anonymous said...

hello, teddy!!
mimi ninashinda na make up ya M.A.C
zinapatikana wapi kwa tanzania kama tu huko USA naomba websit yao niagize asante.

Total Knockout Search!!

Custom Search