Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Sunday, November 15, 2009

Sunday Beauty Tip: Njia ya kuondoa Sugu za Vidole, Magoti na Vipepsi

-Limao
-Sukari
-Mafuta ya mawese

Vitu asilia lakini vinauwezo wa kufanya maajabu kwenye pande za urembo.

Jinsi ya kutumia:
Chukua limao kata vipande viwili, kisha jaza sukari na uanze kusugua kwenye sehemu iliyo na sugu kwa dakika 10. Baada ya hapo osha kwa maji ya vugu vugu.
Kwa matokeo mazuri zaidi waweza kumalizia kwa kujipaka moisturizer au mafuta ya mawese.

Ukifanya hivyo kila siku, kwa kipindi kifupi utaona mabadiliko.

Kazi kwako mdau!

4 maoni / comments:

Anonymous said...

TUPE MAMBO DADA.

disminder.

Anonymous said...

Total Knockout, Asante kwa hiyo tip ya urembo, je ndimu itafanya kazi sawa na ya limau?

Anonymous said...

Once again,asante TK for your Sunday Beauty Tip.Bless!

Anonymous said...

ndimu pia inafaa, mimi nilikuwa na sugu katikati ya kidole cha kati zamani sana early 90s nikaambiwa nisugue ndimu, nyumbani tulikuwaga na zamu mimi na dada yangu yeye anapika wali mimi mchuzi si unajua milo ya bongo? nikawa kila nikisha kupika yale maganda ya ndimu nilotumia kwenye mchuzi nasuguaga kila siku nitakayokuwa nimepika na wala haikuwa kila siku na sugu ilipotea zaidi ya miaka 10 sasa ndo naona kama kipele ile sehemu ilopotea sugu, nitaanza kuisugua tena na vipepsi pia. thanx kutukumbusha TK!

Total Knockout Search!!

Custom Search